Mkuu wa shirika la wakimbizi duniani la umoja wa mataifa UNHCR Bw. Antonio Guterres akitembelea katika moja ya kambi za wakimbizi barani Afrika.
………………………………………………………
Na Mwandishi wetu- Geneva –Swiss.
Shirika la Umoja wa Mataifa la
kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeipongeza na kuihakikishia Tanzania
kwamba linaunga mkono mpango wa Serikali hiyo kuwarejesha nyumbani
wakimbizi kutoka Burundi walioko katika kambi ya wakimbizi ya Mtabila
na kuifunga rasmi kambi hiyo ifikapo mwezi Desemba, 2012
Aidha Shirika hilo la Umoja wa
Mataifa limeipongeza Tanzania kwa kwa jitihada zake za kuwahifadhi
wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu na nchi mbalimbali duniani pamoja
na kudumisha amani nchini humo. Kauli hiyo ilitolewa jana mjini
Geneva Mkurugenzi Mkuu wa UNHCR Bw. Antonio Gutteres wakati wa mkutano
wa Kamati Tendaji(Executive Committee )ya shirika hilo uliofanyika
Geneva Uswisi.
Mkurugenzi huyo wa UNHCR
alihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa UNHCR na Jumuia ya kimataifa
inaunga mkono mpango wa Serikali ya Tanzania kuwarejesha Burundi
wakimbizi wa Kambi ya Mtabila na kuifunga Kambi hiyo ifikapo Desemba 31
mwaka huu. Naye Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt . Emmanuel Nchimbi
alisema kuwa Tanzania inahifadhi jumla ya wakimbizi 100,000 kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) na Burundi ambao wako nchini
kutokana na vita vilivyokuwa nchini mwao.
Aliongeza kuwa katika kutafuta
suluhisho la wakimbizi nchini , Serikali kwa kushirikiana na UNHCR mwaka
uliopita iliendesha mahojiano katika Kambi ya Mtabila inayowahifadhi
wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoko wilayani ya
Kasulu mkoani Kigoma ili kutaka kujua idadi ya wakimbizi wanaotaka
kurejea nchini mwao kwa hiari.
Dr. Nchimbi alisema kuwa mahojiano
hayo yaliyozingatia Sheria ya Kimataifa ya wakimbizi na Sheria za
Kimataifa inahusika masuala ya ubinadamu ambapo wakimbizi 2,400 waliomba
kuendelea kupata hifadhi hapa nchini na hivyo kuhamishiwa kambi
nyingine. Aidha wakimbizi 38,050 walionyesha nia ya kurudi kwao kwa
hiari na hivyo kupewa muda hadi Desemba 31 mwaka huu ili waweze
kujiandaa kurejea katika nchi yao.
Kufuatia hali hiyo Waziri huyo
alitoa wito kwa wadau kuungana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa
wakimbizi hao 38050 wanarudishwa kwao ifikapo Desemba 31 mwaka huu.
Aidha kuhusu suala la wakiingia
nchini mnamo mwaka 1972 , Waziri huyo alisema kuwa bado suala lao
linajadiliwa ili kuangalia kweli wapewe uraia wa Tanzania au
wasipewe. Mhe. Nchimbi aliwashukuru wadau mbalimbali kwa jitihada
zao za kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na wakimbizi na kuahidi
kuendelea kuwapokea wakimbizi watakaohitaji hifadhi nchini Tanzania.
Post a Comment