Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la
Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) linapenda kuwatangazia mapromota,
mameneja pamona na wadau wote wa ngumi katika ukanda huu kuwa kuanzia
leo tarehe 4 Octoba 2012 ubingwa wote wa (ECAPBA) utaishi kwa kipindi
cha miezi minne tu!
Aidha, kuna taratibu mpya za
kuandaa ubingwa wa ECAPBA na wale walio mabingwa mpaka sasa mwisho wa
ubingwa wao ni mwezi wa 12. Baada ya hapo watatakiwa watetee ubingwa na
taratibu mpya za ECAPBA.
1. Kuanzia sasa
mabondia wote watakaogombea ubingwa wa ECAPBA ni lazima wawe
wameshapigana mapambano yasiyopungua 8 mawili ya raundi 4, mawili ya
raundi 6, mawili ya raundi 8 na mawili ya raundi 10.
2. Kabla ya mpambano wenyewe ni lazima majina na rekodi za mabondia watakaocheza zikubaliwe na ECAPBA
3. Waamuzi wote watakaosimamia mapambano haya ni lazima wapitishwe na ECAPBA
4. ECAPBC haitaruhusu pambano kutangazwa kabla ya kupata kibali chake.
Haya yote yanafanyika ili kulinda viwango
na maisha ya mabondia pamoja na wadau wanaoshiriki katika kuuendeleza
mchehzo wa ngumi z a kulipwa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na
Kati.
Imetolewa na;
Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais,
Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)
Dar-ES-Salaam, Tanzania


Post a Comment