NAIBU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema kufeli
kwa baadhi ha wanafunzi kwenye mitihani ya taifa hakutokani na walimu
kutokamilisha mitaala bali kunatokana na uzembe wa wanafunzi wenyewe.
Mulugo alitoa kauli hiyo wakati
akitoa taarifa kwa Umma kuhusu mitihani ya kidato cha nne na mtihani wa
maarifa inaotarajiwa kuanza Oktoba 8 hadi 25 mwaka huu.
Alisema wanafunzi wanaotoa
madai hayo wengi wao ni wale waliyokuwa wakishindwa kuwasikiliza walimu
wao wakati wakifundisha darasani.
“Kwa kawaida mfamaji haishi
kutapatapa hivyo hao wanaosema hivyo mara nyingi ni wale waliyokuwa
wakipata sifuri tangu awali”alisema Mulugo.
Akizungumzia mtihani huo wa
kidato cha nne, Mulugo alisema jumla ya watahiniwa waliondikishwa
kufanya mtihani huo ni 481, 414, wakiwemo vulana 263, 202 ambapo ni sawa
na asilimia 54.67 huku wasichana wakiwa 218, 212 sawa na asilimia
45.33.
Alisema idadi hiyo ya
watahiniwa wote walioandikishwa mwaka huu ni sawa na ongezeko la
watahiniwa 31,090 hiyo ni sawa na asilimia 6.90 ikilinganishwa na
watahiniwa 450,324 walioandikishwa mwaka jana.
Aliongeza kuwa watahiniwa wote
waliondikishwa kufanya mitihani mwaka huu wamegawanyika katika makundi
matatu, ambayo ni watahiniwa wa Shule (School candidates), ni 412,594
wakiwemo wavulana 228,991 sawa na asilimia 55.50, wasichana 183,603
ambapo hiyo ni asilimia 44.50.
Mulugo alisema watahiniwa hao
wa Shule mwaka huu ni ongezeko la watahiniwa 63,204 sawa na asilimia
18.09 ikilinganishwa na na watahiwa 349, 390 wa mwaka jana.
Alisema watahaniwa
wakujitegeamea (Private candidates), ni 68,820 wakiwemo wanaume 34,211
ikiwa hiyo ni sawa asilimia 49.71 na wanawake 34,609 ambapo hiyo ni
asilimia 50.29.
Wengine ni watahiniwa
wakujitegemea walioandikishwa mwaka huu ni pungufu ya watahiniwa 32,114
ikiwa ni upungufu wa asilimia 31.82 ikilinganishwa na watahiniwa 100,
934 walioandikishwa mwaka jana.
Akifafanua zaidi, alisema jumla
wa mtihani wa maarifa walioandikishwa mwaka huu ni 21,314 wakiwemo
wanaume 8,174 hiy0 ni asilimia 38.35 huku wanawake wakiwa 13,140 sawa na
asilimia 61.65.
Mulugo alisema watahiniwa hao
walioandikishwa mwaka huu ni pungufu ya watahiniwa 8,133 sawa na
asilimia 27.62 ikilinganishwa na watahiniwa 29,447 wa mwaka jana.
Wakati huo huo, alisema mwaka
2012/13 jumla ya wanafunzi 11,242 walichaguliwa kujiunga na mafunzo ya
uwalimu, ngazi ya cheti walikuwa 5,615 huku stashahada wakiw 5,627.
Mulugo alisema hadi kufikia
Agosti 30 mwaka huu jumla ya wanafunzi 4,395 ngazi ya cheti na 3,474
ngazi ya stashahada waloripoti vyuoni ambapo wanafunzi 1217 wa ngazi ya
cheti na 2,153 stashahada hawakuripoti vyuoni halioifanya wizara kufanya
uchaguzi wa pili.


Post a Comment