Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imesema itaendelea
kutoa kipaumbele katika kusaidia huduma za jamii nchini kama shemu ya dira ya
biashara ya kampuni hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo
Bw Rene Meza alipokutana na Wahariri Wakuu wa vyombo vya habari nchini jijini
Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kuzungumza na wakuu hao wa vyumba vya habari kwa
lengo la kuzungumzia shughuli za Vodacom hapa nchini.
Amesema katika kuendeleza azma hiyo kampuni ya Vodacom
Tanzania kwa mwaka huu wa fedha imetenga shilingi bilioni mbili na nusu
kufadhili miradi mbalimbali ya kijamii katika maeno makuu manne elimu,afya,
mazingira na uwezeshaji kiuchumi wanawake.
Rene amesema mafanikio ya kibishara ya Vodacom hupimwa
sanjari na namna inavyowekeza katika jamii kupitia kitengo chake cha Vodacom
Foundation jambo ambalo linaifanya kambpuni hiyo kuwa karibu zaidi na
jamii.
Amesema mafanikio ya uwekezaji wake katika jamii – CSR
yameonesha mafanikio makubwa kupitia miradi mbalimbali ukiwemo wa fistula ambao
umeleta staha na faraja kwa wanawake waliokuwa wakisumbumuliwa na tatizo hilo na
mradi wa MWEI.
Akizungumzia huduma ya M-pesa Mkurugenzi Mtendaji huyo
amesema Vodacom itaendelea kuwa makini kuhakikisha mfumo wa huduma hiyo
unaendelea kuwa imara na wa kuaminika sokoni ikitambua nafasi iliyonayo katika
kupunguza tatizo la upatiakanji wa huduma za kibenki
nchini.
Rene amesema ni jambo la wazi kwamba huduma ya M-pesa
imekuwa nguzo muhimu katika maisha ya watu kwa sasa ikitoa urahisi wa kutuma na
kupokea fedha wakati wowote mahali popote hapa nchini kuzindi hata kupitia
mifumo ya kibenki.
Miamala yenye thamani ya kiasi cha shilingi bilioni
moja hupita katika mfumo wa M-pesa kwa siku kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo
mbalimbali.
Kuhusu huduma za mawasiliano Rene amewaeleza wahariri
kwamba kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kuporesha na kupanua upatikanaji wa
huduma itakamilisha mpango wa kujiunga na mkongo wa taifa kwa sehemu kubwa ya
nchi ifikapo Mei mwakani.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa jukwaa la
Wahariri nchini Bw Absalom Kibanda alisema uamuzi wa Rene kukutana na wahariri
kila mwaka unajenga imani na ukaribu kati ya kampuni hiyo na vyombo vya habari
tofauti na wakuu wengi wa makampuni binafsi ambao hawana utamaduni wa kudumu wa
aina hiyo.
Rene aliyejiunga na Vodacom Tanzania Oktoba mwaka jana
alikutana kwa mara ya kwanza na Wahariri Wakuu wa Habari Novemba mwaka jana
ambapo aliwaelezea dira na mikakati yake ya kuhakikisha Vodacom inaendelea
kuongoza soko la huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi
nchini.
Post a Comment