WAFUGAJI
wa Kata ya Msanja wilaya ya Kilindi mkoani Tanga wamesema kuwa licha ya
serikali kuwapa siku 14 kuondoka katika eneo hilo, hawako tayari
kufanya hivyo labda iwatafutie eneo mbadala la kufuga mifugo yao.
Akizungumza kwa
niaba ya wafugaji wenzake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Luis
Qorro alisema kuwa mgogoro unaoendelea katika eneo hilo umesababishwa na
viongozi wa serikali za mtaa kuwadhibiti wakulima pamoja na wafugaji.
Alifafanua kwamba wengi wa
wafugaji na wakulima katika eneo linaloleta mgogoro waliingia eneo hilo
miaka sita iliyopita baada ya seriakli kutoa tamko la kugawa maeneo hayo
kutumika rasmi kwa ajili ya wanakijiji wakiwemo wafugaji.
“Tumeshtushwa na agizo la Mbunge
wa eneo letu kutupa siku 14, huku akitoa kauli kuwa yupo tayari kuuza
kitu chake cha thamani ili kuishinikiza serikali ituondoe hapa, kwa
sababu hiyo basi tunahisi serikali inatunyanyasa maana haikumbuki tamko
lake la awali” kwa mujibu wa Qorro.
Mbali na hilo, alitabanaisha
kuwa mgogoro huo hautaweza kwisha mara moja kwa sababu licha ya
kusababishwa na badhi ya viongozi wa serikali,bado umepandikizwa
chuki,vurugu na wakulima pamoja na wafugaji wenyewe kwa kila kundi kudai
kuwa haliko tayari kuondoka.
Naye Mbunge wa Kilindi Beatrice
Shelukindo(CCM), amekanusha madai hayo kwamba hajafika eneo hilo
takribani miezi mitano, ila kunauwezekano wa Mkuu wa Wilaya hiyo kutoa
agizo hilo kutokana na wengi wao kuvamia eneo hilo kinyemela.
Aidha, alichanganua kuwa
migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima imetawala katika maeneo
mbalimbali nchini, hivyo wilaya hiyo imo mbioni kuwaondoa wale wote
waliovamia maenmeo hayo bila kibali cha serikali.
Post a Comment