Bidzina Ivanishvili. 
Kiongozi wa serikali mpya ya mseto ya Georgia Bidzina Ivanishvili amewataja baadhi ya mawaziri wake, miongoni mwao akiwemo mchezaji wa zamani wa timu ya AC Milan ya Italia Kakha Kaladze na balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa.
Balozi wa zamani kwa Ujerumani Maya Panjikidze ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
Bunge la nchi hiyo sasa linapaswa kuwapitisha mawaziri hao, ingawa hatua hiyo inachukuliwa kuwa ni kutimiza utaratibu tu, kwani muungano wa vyama sita wa “Ndoto ya Georgia“ una viti vya kutosha bungeni. 
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Misri amelazimika kujiuzulu wadhfa wake baada ya Bunge kwa mara ya pili kutaa kupitisha baraza lake la mawaziri.