Viongozi mbalimbali wa Mkoa
wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia waislamu kuacha kuandamana
mara moja.
Katika taarifa ya
waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo
wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, (picha
ya chini) aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli
zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya
amani.
Akitoa tamko hilo, Mkuu
huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu
kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake
amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo
linashughulikiwa kisheria.
Hata hivyo kwa upande wao
viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa juu ya kutolea tamko hilo
waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni
kukiuka misingi mbalimbali ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo
ni kukiuka sheria za nchi.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad
Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza
waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi
iliyopo.Aidha, aliwaomba waumini warejee
majumbani kwa amani.
Askofu Makunda aliwataka
watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya
fujo.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam,
Suleiman Kova (pichani juu) alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo
hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa
amani bila kufanya maandamano na pia
aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida
na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.
“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.
Wakuu hao wamekutana kwa
dharura baada ya kuwepo kwa taarifa za juu ya waumini hao kutishia kuandamana
na kufanya fujo.
Post a Comment