.
KAIMU mkurugenzi wa manispaa ya Arusha Bw. Omary Mkombole amewataka wananchi wa manispaa hiyo ambao wanaishi mabondeni
kuhama mara moja ili kuepusha majanga mbalimbali ya mafuriko ambayo
yatatokana na mvua kubwa za vuli ambazo ziunatarajiwa kuanza hivi
karibuni
Bw. Mkombole aliyasema hayo jana
wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kupokea
taarifa maalumu kutoka mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA)ambayo
ilidai kuwa mkoa wa Arusha utakuwa na mvua nyingi sana
Alisema kuwa kutokana na taarifa
hiyo wananchi wanapaswa kuhama wenyewe tena kwa haraka sana hasa wale
ambao wanaishi katika maeneo ya mabondeni mwa manispaa ya Arusha kwani
endapo kama watakiuka hayo basi watasababisha sana maafa hasa nyakati
hizo za mvua kubwa
Hatahivyo alitaja maeneo ambayo
yanaweza kukabiliwa na maafa ya mafurukio hasa nyakati za mvua kubwa ni
pamoja na maeneo ambayo yapo kwenye miteremko mikali, kwenye makorongo
mbalimbali,ambapo kuanzia sasa wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari ya
kuhama maeneo hayo ambayo wataalamu wamedai kuwa yana kabiliwa na
hatari sana.
Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi
huyo alisema kuwa mbali na tahadhari ya mafuriko pia Halmashauri hiyo
imejipanga kuhakikisha kuwa Mji wa Arusha unakuwa na mpangilio wa hali
juu hususani kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa ambapo wanatakiwa
kuuza bidhaa zao kwa kufuata sheria mbalimbali za majiji ya Kimataifa
duniani
Alisema kuwa kwa sasa Manispaa
hiyo itahakikisha kuwa tatizo la uuzwaji wa bidhaa unafuatwa kwa haraka
sana ambapo wafanyabishara wote wanatakiwa kuuza bidhaa zao ndani ya
maduka yao sanjari na kutumia Mabohari ili kuufanya mji wa Arusha kuwa
katika kiwango cha usafi wa hali ya juu sana
Post a Comment