Na Father Kidevu Blog,
Amboni Tanga
Washiriki wa Shindano la
Redds Miss Tanzania 2012, juzi walikamilisha zira yao ya Kutembelea Mikoa ya
Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga kujionea vivutio vya
utalii katika mikoa hiyo ambapo walimalizia mkoani Tanga kwa kutmbelea Mapango
ya Amboni mkuano humo.
Warembo hao wakiwa katika
mapango hayo ya kale waliweza kujionea vitu mbalimbali ambavyo ni vya kipekee na
vyakuvutia vilivyopo katika mapango hayo ya asili ya zama za
kale.
Miongoni mwa vitu vilivyopo
huko kwenye mapango hayo ni sanamu za aina mbalimbali za Bikira Maria, Maandiko
ya Quran, Daraja, sanamu za jinsia ya kike na kiume, chui, na vitu vingine
mbalimbali vya kuvutia.
Hapa ni katika eneo ambalo linafananishwa na Mlima
Kilimanjaro na hapa warembo wakipanda mlima huo ndani ya Mapango ya asya Amboni
mkoani Tanga.
Wakionesho eneo ambalo linafananishwa na daraja kwa
jinsi lilivyo umbika.
Hapa warembo wakipiga picha katika kiti cha enzi.
Ni jiwe lililochongeka mithili ya sofa na ukiingia pangoni humo inapendeza
kuchukua kumbukumbu.
Eneo hili ni linafananishwa na Mlango wa kupandia
ndege na hapa warembo wakipanda na kutoka nje ya pango.
Bado pango hilo la Amboni linaendelea kukua. Na
hapa warembo wakiangalia moja ya vitu vinavoota kila mwaka hasa wakati wa
mvua.
Hapa huna budi kuinama na huko ndani waweza kuinuka
bila kugusa juu.Wanapotokea..
Warembo wakiangalia moja ya vitu vya kuvutia na
hapa waliangalia mchoro wa asili wa chui aliyelala baada ya
kushiba.
Hakika ukifanikiwa kupita hapa utapita pango
zimana kujionea vitu vingi. Hapa lazima utambae na wengi hushindwa kupenya hapa.
Hata Father Kidevu nilipenya na warembo walishangaa niliwezaje kupenya
kirahisi.
Ni full kushangaa kwa warembo hawa wa Redds Miss
Tanzania 2012. Hakika ni utalii wa ndani uliofanywa na warembo hawa lakini je ni
watanzania wangapi tunatalii katika maeneo ya utalii.
Post a Comment