Katibu Mkuu Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Job Masima akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Ofisini kwake leo alipomtembelea na wajumbe
kutoka JWTZ Makao Makuu waliofika Mkoani Rukwa kwa ajili ya kujionea shughuli
zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni kuzoa
shehena ya mahindi kutoka Mkoani Rukwa kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo
yatasafirishwa kwa reli kwenda Mikoa ya Kaskazini. Jumla ya tani 20,000
zinategemewa kusafirishwa na jeshi hilo ambapo mpaka sasa zimeshazolewa tani
11,000. Mahindi hayo yamenunuliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Chakula.
Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza na ugeni huo Ofisini kwake.
Akizungumza katika kikao hicho Alhaj Chima alilishukuru jeshi hilo kwa kazi
nzuri wanayoifanya kwani mpaka sasa hakuna malalamiko yeyote
yaliyojitokeza.
Baadhi ya maofisa wa
jeshi hilo waliongozana na Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa. Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa
wa Rukwa Samson Mashalla.
Post a Comment