Pichani kati ni
Nakaaya Sumari na wasanii wenzake wakiwa wanamsikiliza Meya wa jiji la Arusha
(hayupo pichani.).
Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya na vikundi mbalimbali vya maigizo mkoani Arusha
wamewataka viongozi wa serikali kutowadharau na kuwashirikisha kikamilifu
katika shughuli mbalimbali za maendeleo jijini hapa
Hali
hiyo imetokea wakati zikiwa zimebaki siku chache ili kufanyika uzinduzi rasmi
wa Jiji la Arusha baada ya wasanii hao kudai kutoshirikishwa kwa lolote
.Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake msanii wa muziki wa kizazi kipya
Nakaaya Sumari alisema kuwa wameshangaa sana kusikia kuwa msanii kutoka dar es
salaam Diamond Platnum atakuja kutumbuiza ilihali wao wapo na hawana
taarifa yeyote.
Nakaaya
alisema kuwa hawana tatizo na Nasibu Abdul(Diamond) ambaye amealikwa kuja
kusherehesha uzinduzi huo ila walichokiona ni dharau kutoka kwa afisa Utamaduni
wa manispaa kwa kutoonyesha ushirikiano na badala yake wamepewa taarifa
ya kufanya kitu juuya uzinduzi huo kama zima moto jana usiku baada ya wao
kuulizia.
“Tumeshanga
sana hii ni dharau wasanii wa arusha hatuheshimiki kabisa na tumeuliza ndo
tunaambiwa eti tuandae kitu kwa ajili ya uzinduzi dah yani inakatisha tamaa
sana alafu afisa utamaduni mwenyewe anatuona anatupotezea”alisema nakaaya
Hata
hivyo Nakaaya alimpongeza Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwa kutoa
ushirikiano wake kwao na kuahidi kushirikiana nao kwa madai ya kilichofanyika
ni makosa ya kibinadamu.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa arusha Hussein Sechonge
alikemea vikali tabia hiyo kwa kuwa wasanii wana mchango mkubwa wa kufikisha
ujumbe na kuwataka viongozi kuwa wazalendo.
Aidha
walimtaka afisa utamadumi manispaa Juma Sule kutoa ushirikiano kwa
wasanii wa hapa kwa kuwa wao ndio wanajua kila kitu kuhusu manispaa na sio
Diamond. ”tunamshangaa sana hapa kuna wasanii 70 sasa nashangaa kwenye
mwenge aliletwa Juma Nature wakati wao wapo hapa na hawafahaamu kitu chochote
sio vizuri”alisema Sechonge
Hadi
jamii blog inaondoka katika ofisi za manispaa wasanii hao
walikuwa nje ya ofisi ya meya wakisubiri kujadiliana namna ya kufanya na
kumaliza tofauti hiyo.Habari kwa hisani ya http://pamelamollel.wordpress.com/
on Wednesday, October 31, 2012
Post a Comment