THE UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete aelekeza viongozi kushughulia njaa
Kilimanjaro
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameuelekeza
uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro na hasa Wilaya ya Same kufanya tathmini kamili na
ya haraka kujua kiwango cha njaa katika wilaya hiyo ili kuiwezesha Serikali
kutoa chakula cha msaada ama cha bei nafuu kwa wananchi.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaipatia jawabu la kudumu changamoto ya
maji katika maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro na hasa Wilayani Same.
Rais
Kikwete alitoa agizo la kushughulikia tatizo la njaa jioni ya jana, Jumatatu,
Oktoba 29, 2012, wakati alipoelezwa na wananchi katika maeneo mbali mbali ya
Wilaya ya Same aliposimama mara kwa mara kusalimia wananchi kwenye siku ya pili
ya ziara yake ya siku nne Mkoani Kilimanajaro.
Wananchi
katika maeneo ya Hedaru na Lembeni walimwambia Mheshimiwa Rais Kikwete kuwa
wanakabiliwa na njaa kwa sababu ya ukame ambao umesababisha wasipate chakula cha
kutosha kwa miaka mitatu iliyopita.
Baada
ya kusikiliza malalamiko hayo hasa kuhusu njaa na ukosefu mkubwa wa maji, Rais
Kikwete alisema: “Nimesikia maelezo yenu kuhusu ukosefu wa
chakula na njaa. Mkuu wa Mkoa yupo hapa pamoja na Mkuu wa Wilaya na napenda
kuwaagiza wafanye tathmini ya haraka kuhusu kiwango cha tatizo ili Serikali
ichukue hatua ya kumaliza tatizo hili.”
Aliongeza
Mheshimiwa Rais: “Hakuna wasiwasi. Hakuna mtu ambaye
atapoteza maisha yake kwa sababu ya njaa. Tunacho chakula cha kutosha na
Serikali itahakikisha chakula kinapatikana mara tu tathmini
itakapokamilika.”
Aliongeza
Rais Kikwete: “Chakula kitakuwa cha aina mbili. Kwa familia zisizokuwa na uwezo
kabisa chakula kitatolewa bure. Kwa wale wanaojiweza, chakula kitatolewa kwa
wananchi kuchangia fedha kidogo sana kama Sh. 50 tu.”
Rais
Kikwete alisimamishwa mara tisa na wananchi ambao walikuwa na hamu ya kumwona na
kusalimiana naye akiwa njiani kutoka
Mamba Miamba ambako alizindua Kiwanda cha Kusindika Tangawizi kwenda
Mwanga ambako alifungua Hosteli ya Shule ya Wasichana ya Asha Rose Migiro mjini Mwanga.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es
Salaam.
30 Oktoba, 2012
Post a Comment