Mama Beatrice Martin
(pichani) mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani ambaye ana matatizo ya uvimbe mkubwa
kwenye mguu wake wa Kulia kwa takribani miaka 15 uliyosababisha ashidwe kufanya
shughuli yeyote ile ya maendeleo binafsi na akiwaomba watanzania waendelee
kumsaidia kwa hali na mali ili aweze kujiunga na watanzania wenzake katika
shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mama Martin anasema mpaka
sasa ana kiasi cha shilling Millioni 8 benki na baada ya Mwandishi wa Habari kwa
Kituo cha ITV kumkabidhi Million 4 sasa amefikisha Millioni 12 na ushee benki,
kwa mujibu wa maelezo yake ameshawasiliana na madaktari wa hospitali ya Apollo
nchini India na wamemhakikishia kwamba kuna uwezekano wa yeye kutibiwa bila
kukatwa mguu lakini zinahitajika Millioni 27 fedha za
kitanzania.
Kwa Mtanzania atakayetaka
kuchangia kwa ajili ya matibabu ya mama huyu unaweza kutuma kupitia 0716- 850350
au 0767850351au account number 011201364730 NBC.


Post a Comment