Mahmoud Ahmad -Arusha
………………………………….
Akizungumza na
Fullshangweblog.com Meneja mahusiano wa shirika hilo Pascal Shelutete
alisema kuwa Tanzania imebahatika kuingiza vivutio hivyo na kuwataka
Watanzania kuipigia kura vivutio hivyo kwani Serengeti imeweza kingizwa
kwa sababu ya kuhama kwa wanyama aina ya nyumbu,kwani ni tukio adimu
hapa ulimwenguni.
Alisema kuwa wapiga kura
wanatakiwa kuchagua vivutio hivyo na kuvipigia kura iliviweze kupita na
pia unatakiwa kuongeza vivutio vingine 4 unavyovifahamu ilikuweza kupata
vivutio saba vilivyopo barani Afrika na kuuelezea mlima Kilimanjaro upo
kwenye mstari wa tropiki na ni joto lakini unatheluji ambayo haikauki
kwa majira yote.
Shelutete alisema kuwa
utaratibu wa kupiga kura unatumika kwa kutumia barua pepe na kuwa wao
kama tanapa wanashirikiana na wadau mbali mbali nkuweza kuona kuwa
Tanzania inaingizwa kwenye moja ya maajabu hayo saba.
Aidha alisema kuwa mbali na
kuwataka kupiga kura pia wanaendelea kuwahamasisha watanzania
wakishirikiana na wadau mbali mbali ilikuweza kuwafahamisha watapata
faida gani watanzania ilikuweza kuwahamasisha wale wote waliotembelea
kwenye mbuga wakiwa ni wageni na watanzania kuweza kupigia kura vivutio
hivyo.
Shelutete Faida tunayoipata ni
kuendele kuvitangaza vivutio hivyo kwenye mataifa mbali mbali hivyo
tutaweza kuongeza wageni watakaokuja kutembelea vivutio hivyo na
kuongeza pato la uchumi na la taifa hadi sasa waratibu wa shindano hili
hawajatoa nani yupo kwenye nafasi ipi lakini tunaimani kuwa hadi ifikapo
mwezi wa December ambapo shindani hilo litafikia tamati ya upigaji kura
tunaimani nasi tutakuwa ni mojawapo ya maajabu hayo ya afrika.
Shelutete alisema kuwa Shindano
la kuchagua maajabu saba ya Afrika limeandaliwa na shirika la Seven
Natural Wonders lenye makao yake makuu Texsas Nchini marekani na
madhumuni ya shindano hili ni kutafuta maajabu saba ya Ulimwengu na
kutoa sifa ya mbuga ya Serengeti ambapo kwa miezi 12 wanyama wanahama
kutoka eneo moja kwenda nchi kufuta malisho.


Post a Comment