Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WIZARA YA MAL ASILI NA UTALII INAJIVUNIA UTHIBITI WA UHIFADHI WA TEMBO

Aliyekuwa  waziri wa Maliasili na utalii Bw Ezekiel Maige akitazama meno ya tembo yaliyokamatwa na askari  wa wanyamapori ,chini waliokamatwa ni majangili

Wizara ya Maliasili na utalii imeongeza idadi ya askari na silaha zitakazotumika kukabiliana na ujangili katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa ujangili hauathiri maisha ya tembo na wanyama wengine nchini.
Katika kuhakikisha hilo Wizara imeweka utaratibu wa kupata matukio ya kila siku kutoka vituo vyote vya hifadhi kuhusiana na ujangili wa wanyamapori wote akiwemo tembo.
Wizara pia inafuatilia taarifa za mienendo ya tembo chini ya Taasisi yake ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kuanzia kipindi cha Mwaka 2010 hadi 2015.  Kazi kubwa ya taasisi hii ni kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na maisha ya tembo kwa kuangalia uzao, mtawanyiko, maradhi, malisho na vifo vya tembo kwa ujangili, maradhi au umri ikiwa ni pamoja na kufanya sense za wanyamapori wote.
Taarifa za TAWIRI zinaonesha kuwa idadi ya tembo bado ni kubwa na vifo vilivyoripotiwa vya ujangili bado viko kwenye kiwango cha kawaida.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top