Naibu
waziri wa maliasili na utalii Mhe.Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi
wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam kuhusu kukamilika kwa
maandalizi ya mkutano mkuu wa kwanza wa Africa katika usimamizi wa
utalii endelevu utakaofanyika mkoani Arusha katika ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Arusha (AICC)kuanzia tarehe 15-18 mwezi huu mwaka 2012.
Mkutano huo utajumuisha wajumbe
412 kutoka nchi 40 za Africa ambapo asilimia 59 ya wajumbe hao wanatoka
Tanzania na asilimi 41 ya wajumbe wanatoka nchi nyingine za Africa mgeni
rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa makamu wa Rais wa jamuhuri wa
muungano wa Tanzania Mh. Dr Mohamed Ghalib Bilal.wadau na watanzania
kwa ujumla wametakiwa kwenda kuunyesha mali asili zao wanazotengeneza
ili kujipatia soko na kujitangaza kupitia mkutano huo
Post a Comment