ABIRIA wanaotumia usafiri wa treni Dar, juzi walimtoa kijasho Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alipokwenda kuwasimamia abiria hao wapande kwa foleni kwenye treni inayotoka Stesheni kwenda Ubungo Maziwa.Dk Mwakyembe aliwasili eneo hilo kati ya saa tisa alasiri na saa kumi na moja jioni kushuhudia usafiri huo unavyoendelea, ambapo alikutana na kadhia mbalimbali kwenye huduma hiyo mpya jijini.
Alitumia kipaza sauti kutoa maagizo kwa abiria kusimama kwenye foleni, lakini jitihada zake zilichukua muda kueleweka kwani kadri alivyokuwa akitangaza ndivyo abiria hao walivyomzonga.
“Nasema simameni kwenye foleni, kama mtu hatasimama kwenye foleni hatapanda” alisema Dk Mwakyembe mara kwa mara lakini abiria badala ya kufanya kile alichowaagiza walikuwa wakimsonga
on Monday, November 5, 2012
Post a Comment