Abiria zaidi ya 40 wamenusurika kufa baada ya basi dogo aina ya Costa lenye namba za usajili T.333 BNK lililokuwa linatoka Singida mjini kwenda kijiji cha Ilunda wilayani Iramba, kupinduka katika eneo la kituo cha mabasi cha zamani kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuzidiwa na uzito wa mizigo iliyokuwa imepakiwa.
Picha mbalimbali zinazoonyesha basi hilo kupinduka.