Mwili wa kiongozi wa zamani wa Mamlaka ya Palestina Yasser Arafat umeanza kufukuliwa katika eneo alikozikwa kwenye mji wa Ramallah Ukingo wa Magharibi.
Arafat alifariki dunia katika hospitali ya kijeshi nchini Ufaransa mwaka 2004, lakini madaktari wa Ufaransa hawakueleza chanzo cha kifo chake.
Wachunguzi wanataka kubaini chanzo cha kifo hicho kuona kama alikufa kutokana na sumu ya mionzi ya madini ya polonium.
Taasisi ya matibabu ya Uswisi iligundua aina ya chembechembe za madini kwenye vifaa binafsi vya Arafat.
Timu ya wataalamu wa Ufaransa, Uswisi na Urusi wanatarajiwa kuchunguza sampuli za mwili wa Arafat kutoka kwenye kaburi lake, mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba.