Wachezaji Taifa Stars |
TIMU ya soka
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeibwaga Kenya, Harambee Stars bao 1-0
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza jioni hii katika mchezo wa kirafiki
ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hadi
mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki Aggrey
Morris katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia
mashambulizi.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa anayetambuliwa na FIFA, Oden Mbaga, Kenya walitawala
dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo Stars wakafunguka nao na kuanza kula
nao sahani moja na Harambee Stars.
Kipindi cha
pili, Kenya walianza na mabadiliko kocha Henri Michel akiwapumzisha James
Situma, Jerry Santo na Wesley Kemboi na kuwaingiza Christopher Wekesa, Anthony
Akumu na Timbe Ayoub.
Pamoja na
mabadiliko hayo, mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Harambee Stars, kwani wenyeji
waliendelea kucheza kwa makini, wakishambulia na kujilinda
zaidi.
Kocha wa
Stars naye, Mdemnark, Kim Poulsen aliwatoa Amir Maftah, Salum Abubakar, Mwinyi
Kazimoto, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu na kuwaingiza Nassor
Masoud ‘Chollo’, Amri Kiemba, Simon Msuva, John Bocco ‘Adebayor’, Shaaban Nditi
na Issa Rashid.
Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Kenya anayechezea
AJ Auxerre ya Ufaransa alifichwa kabisa na mabeki wa Stars.
Baada ya
mchezo huo, kocha wa Harambee, Mfaransa Michel alionyesha kukerwa na matokeo
hayo na kusema timu yake haikucheza vizuri, wakati Polusen, amefurahia ushindi
huo akisema timu yake haijacheza kwa miezi miwili na baada ya siku mbili za
mazoezi wameifunga Kenya.
Taifa Stars; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah/Nassor
Masoud ‘Chollo’ dk70, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum
Abubakar/Amri Kiemba dk69, Mwinyi Kazimoto/Simon Msuva dk69, Mbwana Samatta/John
Bocco dk 84, Mrisho Ngassa/Shaaban Nditi dk72 na Thomas Ulimwengu/Issa Rashid dk
89.
Harambee
Stars; Frederick
Onyango, Brian Mandela, Eugene Asike, James Situma/Christopher Wekesa dk 46,
Edwin Wafula, Jerry Santo/Anthony Akumu dk 46, Peter Opiyo/Charles Okwemba dk
67, Patrick Obuya, Patrick Osaika/Mulienge Ndeto dk 73, Dennis Oliech na Wesley
Kemboi/Timbe Ayoub dk 46.
Post a Comment