Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la UNESCO (kesho) jumamosi tarehe 17 Novemba watazindua rasmi radio ya jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya ametaarifu kuwa sherehe ya uzinduzi wa radio hiyo ya kijamii inatarajiwa kuhudhuriwa na mgeni wa heshima Waziri wa Mawasiliano nchini Profesa Makame Mbarawa katika kijijini cha Ololosokwani Akiendelea kuelezea alisema "Airtel na Unesco wanatimiza dhamira waliojiweke ya kuwafikia na kusaidia jamii zilizopo pembezoni hasa wakina mama ambao katika jamii hizi wamekuwa wakiachwa nyuma katika mambo mengi na mwisho wake kutotambua nafasi zao"
Singano alisema "Mradi huu utasaidia kupigana na kutokomeza changamoto za mila zilizopitwa na wakati zikiwemo ukiketwaji wa wanawake, elimu duni, imani za kishirikina, umaskini ,unyanyasaji wa kijinsia, kukua kwa kasi kwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine maandalizi ya sherehe ya ufunguzi yamekamilika na kubainisha kuwa wananchi wa vijiji vyote jirani na ololosokwani takribani vijiji 14 watafaidika pia kwa kujipatia huduma bora kutoka Airtel ikiwemo ile ya
Airtel Money pesa mkononi wakati wowote kijijini hapo alimaliza kusema Bi, Singano
Akifafanua kuhusu ufungwaji wa Mitambo hiyo ya radio, Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin amesema "mradi wetu wa kijamii umekamilika, tunawashukuru Airtel na wananchi wote kwa ushirikiano wao wa kutuunga mkono kukamilisha lengo, mitambo hii ya mawasiliano utatoa fulsa kwa wakazi wote wa ololosokwani na vjiji jirani kujifunza mambo mapya, pia tunaanzisha multimedia center ambayo utawaweza wakazi wa kijiji hapa kutembelea tovuti mbalimbali, na kuunganishwa na mtandao wa kisasa wa intaneti ya Airtel"
Sehemu nyingine zitakazonufaika na mradi huo wa radio za kijamii ni pamoja na Sengerema Mwanza, Karagwe Kagera, Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja, Pangani Tanga, Kyela Mbeya and Kalama Shinyanga.
Post a Comment