Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Lilly Matola akielezea tukio lenyewe
lilivyokuwa.
SMG
yenye namba T 1964 TB 8799.
Mkutano na Waandishi wa Habari.
JESHI la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi watuhumiwa wawili wa ujambazi na kufanikiwa kukamata bunduki moja aina ya Sub Machine Gun (SMG), ikiwa na risasi 43.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lilian Matora, alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kumkia jana katika eneo la Kilimahewa Big Bite, Nyamanoro jijini hapa.
Polisi wakiwa katika doria ya kawaida, walishambuliwa kwa risasi na majambazi watano waliokuwa katika harakati za kupora wananchi mara baada ya polisi hao kupita katika mtaa husika na kugundua kuwa kuna hali ya utata isiyoeleweka.
Alisema polisi walijipanga vizuri na kufanikiwa kujibu mapigo ambapo majambazi wawili waliuawa papohapo kwa kupigwa risasi ambapo katika tukio hilo, majambazi wengine watatu walifanikiwa kutoroka.

Post a Comment