Jamaa mmoja mwenye asili ya Lebanon amekamatwa nchini Afrika Kusini wakati akisubiri kupanda ndege katika kiwanja cha ndege cha jijini Johannesburg kuelekea Dubai.
Polisi nchini Afrika Kusini wamesema jamaa huyo alikuwa amemeza vipande 220 vya almasi kwa nia ya kuvisafirisha nje ya nchi hiyo.
Maafisa hao wamesema kipimo cha picha ya mwili wake kilionyesha vipande hivyo vya almasi vyenye thamani ya Dola za Marekani milioni 2.3, sawa na paundi milioni milioni 1.4 za Uingereza au Euro milioni 1.8 za Umoja wa Ulaya ambazo ni takribani zaidi ya shilingi milioni 355 za Tanzania.