Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania
Amour Zacarias Kupela (kulia) Picha maktaba
Aliyekuwa Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania
Bw.Amour Zacarias Kupela amekabidhi msaada wa vifaa vya Kusomea vyenye thamani
ya Shilingi Milioni 1.2 kwa wanafunzi 500 wa Shule ya sekondari masonya zikiwa
ni juhudi za nchi yake kudumisha urafiki na
Tanzania.
Msaada huo uliotolewa na kiongozi huyo ni
madaftari makubwa (Counter Book 500), Peni 500 na Pensel 500 na Mipira 5
umetolewa kutokana na mapenzi ya Balozi huyo ambaye pamoja na mambo mengine
ameahidi kuenzi kumbu kumbu za wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji na eneo
ambapo ilianzishwa Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa Msumbiji (OMM) march
16/1973.
Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Balozi
Kupela katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania
Bw.Daniel Rui Simao Ntada alisema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa ahadi ya
Balozi huyo aliyo itoa wakati alipofanya ziara ya kuaga viongozi wa Wilaya ya
Tunduru ambapo aliahidi kuisaidia Shule hiyo iliyopo katika eneo la kambi ya
wapigania uhuru wa Chama Cha Frelimo Nchini Msumbiji
.
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Rui alisema kuwa
Balozi Kupela alitoa ahadi hiyo wakati alipotembelea katika eneo hilo muhimu kwa
historyia ya wapigania uhuru wa Nchi yao ambapo palikuwa ni miongoni mwa kambi
kubwa za wapigania uhuru wa nchi yao wakiwemo Kamarada Samora Machel, Marcelino
Dos Santos, Rais wa sasa Armando Guebuza, Dkt. Edward Mondlane na wengine
wengi.
Katika taarifa hiyo pia Bw. Rui kwa niaba ya
Balozi Kupela alisema Msaada huo ni juhudi za Balozi huyo kuendeleza kudumisha
urafiki wa nchi hizo pamoja na kutunza, kuyahifadhi maeneo yote ya kumbu kumbu
na kuenzi historia ya Tanzania na Msumbiji.
Bw. Rui alibainisha kuwa Kwavile Chama cha
Frelimo Kilianzishwa Tanzania kwa kutoa baadhi ya maeneo ya ardhi yake kwa Chama
hicho Cha Frelimo ambapo wapigania Uhuru hao walijenga Kambi za Kijeshi katika
maeneo ya Nachingwea,Kongwa,Bagamoyo,Masonya na katika Hospitali ya Ligula
Mkoani Mtwara ili wapigania uhuru waendelee kutibiwa .
Mwl. Ngaunje katika hotuba yake pia alipokea
mwaliko wa kupeleka Wanafunzi wa Shule yake katika Ziara ya kubadilishana
taaluma katika Shule ya Sekondari Mekula iliyopo Mkoa wa Niasa
Nchini Msumbiji
Wasemaji wengine katika hafla hiyo walikuwa ni
Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Tunduru Mwl. Ally Mtamila mwakilishi
wa Afisa elimu Shule za Msingi Wilayani humo Mwl. Kerlen Kitosi ambao pamoja na
kumpongeza Balozi Kupela kwa msaada huo pia walipongeza juhudi zake za
kuendeleza elimu ya Tanzania.
SOURCE: DEMASHONEWS
BLOG
Post a Comment