Balozi wa Japan Mr. Masaki
Akodo
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada kesho
anataraji kutia saini makubalino ya msaada wa fedha kiasi cha shilingi Milioni
380 kwaajili ya miradi miwili ya ujenzi wa bweni La Wasichana pamoja na Shule ya
watoto wenye ulemavu katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ubalozi huo
jijini Dar es Salaam, inasemakuwa miradi hiyo ni upanuzi wa shule ya wenye
ulemavu Dinyecha Wilayani Mtwara utakao gharimu zaidi ya shilingi Milioni 192 na
ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu shilingi
Milioni 188.
Miradi hiyo miwili
inasimamiwa na taasisi za Tanzania Life Improvement Association (TALIA) ya
Mtwara na Women in Social Entrepreneurship (WISE) ya mjini
Lindi.
Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umekuwa ukichangia
fedha katika miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta ya Afya, elimu na maji
tangu mwaka 1991 ambapo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita mikoa ya Lindi na
Mtwara imepatiwa msaada katika miradi 71 iliyogharimu dola za kimarekani
6,135,418 sawa na shilingi Bilioni 9,614,629485.
Utiaji saini huo utafanyika katika ofisi za mkuu wa
Mkoa wa Lindi na Mtwara kati ya saa 3 asubuhi na saa 5.
on Tuesday, November 6, 2012
Post a Comment