Fauzia Yusuf Haji Adan (pichani) ni mmoja wa wanasiasa kumi waliteuliwa katika baraza la mawaziri ambalo ni ndogo sana na ameteuliwa kama waziri wa mambo ya nje.
“Baada ya majidiliano ya muda mrefu na kushauriana , nimeteua baraza la mawaziri, ambalo linajumuisha mawaziri kumi. Miongoni mwao ni waziri wa kwanza mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya Somalia’’ alisema waziri mkuu Bwana Shirdon.
“Uteuzi wangu kama waziri wa mambo ya nje ni jambo la kihistoria kwa Somalia na hasa kwa wanawake , inafungua ukurasa mpya wa siasa za nchini humu na tutafanikiwa katika uongzi wetu.’’ Alisema bi Adan
Bi Adan anatoka katika jimbo la Somaliland lililojitenga na ameishi nchini uingereza kwa miaka mingi.
Changamoto kubwa inayokabili serikali mpya inayoungwa mkono na Umoja wa matifa, ni wapiganaji wa Al shabaab, lilokwishafanya mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu.