Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo na Mali Asili Ndugu Juma Ali Juma na Ofisa wake wa Kilimo wakimuonyesha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif eneo la Ramani ya Shamba la
Wizara hiyo la ekari 6 linaloleta mzozo wa umiliki.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuonyesha Mkurugenzi wa Kituo cha Kujiendeleza
Kielimu Kilichopo Selemu Ndugu Kassim Hassan Nyaraka zake alizozigushi za
umiliki wa eneo la shamba la Kilimo katika Kijiji
hicho.
Bwana Abeis Said Shankar
anayemiliki shamba katika eneo la Selemu akijitetea mbele ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kulalamikiwa ukorofi anaowafanyia
wana kijiji wa hapo katika shughuli za Kilimo na Ufugaji.
Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imeamua kumfutia mara moja hati ya umiliki wa Eneo la Shamba la
Serikali Bwana Abeid Said Shankar alilopewa katika Kijiji cha Sehemu kufuatia
mgongano unaoendelea kujitokeza kati yake na Wana kijiji wa eneo hilo ambao
unaashiria hatma mbaya ya kuvunjika kwa amani baina ya pande hizo
mbili.
Serikali pia imeuzuia
Uongozi wa Kituo cha Kujiendeleza Kielimu cha Eneo hilo kufanya shuguli yoyote
ya ujenzi kwa vile umiliki wake hauko kihalali katika vyombo vinavyosimamia
masuala ya Ardhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara fupi
katika eneo hilo ambapo alishuhudia mgongano na malalamiko ya Wananchi hao
dhidi ya wawaoendesha na Kumiliki Mashamba na Maeneo
hayo.
Mama Mmoja alietaka kujenga
nyumba katika eneo la Kituo hicho cha Kujiendeleza Kielimu baada ya kuombewa
ruhusa na Uongozi wa Shehia hiyo alijikuta akizuiwa kujenga na Mkurugenzi wa
Kituo hicho Bwana Kassim Hassan Juma ambaye alikuwa na nyaraka sizizo halali
zinazokisiwa kuwa ni za kughushi.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara Kilimo na Mali asili Ndugu Juma Ali Juma ambaye alikuwepo kwenye mkutano
huo alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Bwana
Kassim Hassan hakuwa na Nyaraka halali za eneo hilo ambalo ni milki ya Wizara
ya Kilimo.
Ndugu Juma alisema
kutokana na maombi na umuhimu wa Ardhi kwa mahitaji ya Jamii Serikali
imeshaiagiza Wizara hiyo kulipima eneo hilo ili baadae ligaiwe kwa Wananchi kwa
kuendeleza mahitaji yao Kilimo na Ujenzi ambapo alieleza kuwa kazi hiyo
imeshakamilika.
Aidha Balozi Seif
aliendelea kuiasa Jamii kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali ili
kuwepuka mizozo isiyokuwa na lazima na kutahadharisha kwamba ardhi itaendelea
kuwa mali ya Serikali na itakapoamua kuitumia ardhi hiyo kwa maslahi ya umma
haitasita kufanya hivyo mara moja.
Eneo hilo la Ekari sita
liliopo katika Kijiji cha Selemu kilichojaaliwa utajiri wa ardhi ya Rutba liko
chini ya Umiliki wa Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar tokea mwaka
1964.
Post a Comment