Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VIONGOZI WA AFRIKA WATOA WITO KWA WAPIGANAJI WA M23 KUONDOKA KATIKA MJI WA GOMA DRC.

 


Wacongo wakimbia vita kutoka mji wa Sake, 27km magharibi ya Goma, Nov. 23 2012.
VIONGOZI wa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati walikutana Jumamosi mjini Kampala kujaribu kutanzua mzozo unaoendelea mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkutano huo ulohudhuriwa na Marais wa Uganda, Tanzania Kenya na Congo ulipendekeza mpango wenye nukta nane, juu ya jinsi ya kutanzua mzozo huo.

Rais Paul Kagame ambae anatuhumiwa na ripoti ya Umoja wa Mataifa kwamba anawafadhili wapiganaji wa M23 hakuhudhuria mkutano na katika dakika za mwisho alimtuma waziri wake wa mambo ya nchi za nje, Bibi. Louise Mushikiwabo.


Viongozi hao wamewataka pia waasi wa kundi la M23 kusitisha mara moja mashambulizi yao na kuondoka Goma. Wamependekeza pia kuwepo na kikosi cha kimataifa kwenye uwanja wa ndege wa Goma ikiwahusisha majeshi ya Tanzania na DRC


Umoja wa mataifa imeituhumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi hao wa M23, jambo Kigali inakanusha.

Mkutano huo wa viongozi mjini kampala umefanyika kukiwa na wasi wasi kwamba waasi wanasonga mbele huko mashariki ya nchi na kukiwepo na mabadiliko katika jeshi la Congo.

Kwa upande mwengine mashirika ya misaada ya dharura yanaeleza wasi wasi wao kutokana na ukatili unaotendewa raia ambao wengi wako njiani wakikim bia vita.

Kuna ripoti za maiti kuonekana njiani kati ya Goma kuelekea upande wa kusini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top