Papa Benedict
amewatawaza makadinali sita wepya, kwenye sherehe iliyofanywa
Vatikani.
MMOJA baada ya mmoja, wanaume sita kutoka Libnan,
India, Nigeria, Philippines, Colombia na Marekani - walipiga magoti kuvishwa
kofia nyekundu na pete ya wadhifa wao.
Mwandishi wa BBC
alioko Vatikani, anasema makadinali hao wameteuliwa baada ya malalamiko kutoka
viongozi wa kanisa la Katoliki katika nchi zinazoendelea, kwamba makadinali
walioteuliwa awali mwaka huu walikuwa wengi wazungu, hasa Wataliana wanaotumika
Vatikani.
Kwa mara ya
kwanza hakuna mzungu wala Mtaliana kati ya makadinali wepya.
Lakini wazungu
ndio wengi ndani ya baraza kuu la makadinali 120 ambalo ndilo humchagua papa
mpya.
Mtindo unaelekea
kuwa na kanisa litalowakilisha wafuasi wake ulimwenguni.
Papa
aliwakumbusha makadinali wepya kwamba kofia na makoti mekundu wanayovaa ni alama
kuwa wamejitolea kumwaga damu kutetea imani yao ikihitajika.
Papa Benedict
piya alisisitiza kuwa Kanisa Katoliki ni la binaadamu wote wa utamaduni na
makabila yote.
Uamuzi wa Papa wa
kuteua makadinali kutoka nchi tatu zenye Waislamu wengi, yaani Libnan, Nigeria
na India, unaonesha ana wasiwasi juu ya uhusiano baina ya Ukristo na
Uislamu.
Kadinali kutoka
Libnan ni kasisi wa kati ya makanisa kongwe kabisa Mashariki ya
Kati.
Askofu wa Abuja,
kadinali mpya kutoka Nigeria ambako nusu ya wananchi ni Waislamu, anaweza
pengine siku moja kuwa papa wa kwanza kutoka Afrika.
Post a Comment