SERIKALI ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo inasema
haitazungumza na wapiganaji wa M23 hadi waondoke mji wa Goma ambao waliuteka
juma lilopita.
Taarifa hiyo
imetolewa siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu mjini Kampala,
Uganda, kuwasihi wapiganaji waondoke Goma.
Msemaji wa
wapiganaji, Kasisi Jean-Marie Runiga, alisema wapiganaji wataondoka Goma baada
ya mazungumzo ya amani lakini siyo kabla.
Rais Joseph
Kabila wa Congo alikutana na wawakilishi wa wapiganaji mjini Kampala
Jumamosi.
Wakuu wa Uganda
wanasema yamekuwapo mawasiliano baina ya pande hizo mbili.
Post a Comment