DURU za habari kutoka
Libya zinaripoti juu ya kuzimwa jaribio la
mapinduzi ya kijeshi
yaliyopangwa na maafisa wa zamani wa jeshi la
nchi
hiyo.
Taarifa zinasema kuwa,
kundi la kwanza la maafisa hao tayari
limeshakamatwa katika
mji wa Benghazi mashariki mwa nchi hiyo,
huku shirika la kijasusi
la kijeshi la Libya likiendelea na msako wa
kuwatia mbaroni viongozi
wengine wa mtandao huo huko Tripoli.
Hii ni mara ya kwanza
kutokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini
Libya tokea
alipong'olewa madarakani dikteta Kanali Muammar
Gaddafi.
Hivi karibuni kumetokea
mauaji yanayofanywa na watu
wasiojulikana dhidi ya
viongozi wa kisiasa na kijeshi nchini humo,
miongoni mwao wakiwemo
AbdulFattah Younnis aliyekuwa
Kamanda wa Operesheni za
kijeshi dhidi ya vikosi vya Gaddafi
katika kipindi cha vita
vilivyotokea mwaka uliopita nchini humo,
na Kanali Faraj al
Darsi Kamanda wa Usalama wa Benghazi.
Post a Comment