Mapenzi ya ROMAN ABRAMOVICH na straika mwenye
jina kubwa kwa mara nyingine yamemgharimu kazi kocha mwingine wa
Chelsea.
Roberto Di Matteo alitimuliwa saa nne asubuhi akitokea nchini Italia
alipoiongoza Chelsea kudungwa 3-0 na Juventus, Fernando Torres amecheza part
kubwa sana katika kufukuzwa kazi kwa makocha watatu waliopita wa The Blues - Di
Matteo, Andre Villas-Boas na Carlo Ancelotti.
Ungeweza kufikiria kwamba
Abramovich anaweza alijifunza kitu kutoka kwenye sakata la Andriy
Shevchenko.
Jose Mourinho, akijiandaa kwa msimu wa wa 2006-2007 baada ya
kushinda ubingwa wake wa pili, akasajiliwa mchezaji ambaye hakuwa hata
akimtaka.
Lakini mmiliki wa kirusi aliendelea kumng'ang'ania: "Ni mchezaji
wangu mwenye gharama ya £30million na yupo kwenye timu.
Mahusiano ya Mourinho
yakaharibika na hawakuweza kuwa vizuri tena.
Mpaka Mourinho anatimuliwa baada
ya michezo sita ya msimu wa 2007-2008, Shevchenko alikuwa amefunga mabao manne
katika premier league ndani ya michezo 31 - na hatimaye aliondoka Stamford
Bridge akiwa amefunga mabao 9 katika mechi 48.
Abramovich, akaendelea kuwa
mbishi.
Na historia ikajirudia tena kwa Fernando Torres.
Akitiwa upofu na
rekodi nzuri ya magoli ya mhispania alipokuwa Liverpool ingawa katika mwaka wake
wa mwisho hakuwa kwenye kiwango kizuri, Abramovich akaweka mezani £50million
mwezi January 2011 kwa matumaini Torres angeongeza makali katika kikosi cha
Carlo Ancelotti kilichoshinda makombe mawili.
limekuwa janga
lisilotibika.
Torres alienda na kufunga bao 1 tu katika mechi 14 za ligi na
hakupata chochote katika champions league ambapo Chelsea walitolewa na
Manchester Unitedo fainali. Ancelotti nae akaenda na maji.
Akaingia AVB ambaye alianza
kwa kuleta mabadiliko ndani ya kikosi - jaribio ambalo lilidumu kwa mechi 27
huku Torres akifunga mara moja tu katika mechi 22. Akatimuliwa AVB.
Na sasa
ameondoka Di Matteo. Katika mechi kadhaa zilizopita ambazo mambo yamekuwa magumu
kwa Di Matteo - Torres hakuwa kwenye kiwango kizuri kabisa. Hakuna la
kushangaza.
Pamoja na jitihada zote za meneja kumpa nafasi nyingi kadri
iwezekanavyo lakini wachezaji wenzake wameshapoteza matumini nae - kiasi kwamba
Di Matteo alijaribu kumuacha katika kikosi chake kilichocheza Turin dhidi Juve
japokuwa alionywa kwamba jambohilo lingempotezea kazi yake.
Di Matteo siku
zote amekuwa ni jaribio kwa Abramovich. Kwanza kabisa hakuwahi kumtaka kwenye
nafasi ya kocha mkuu hasa pale aliposhinda Champions league - na hilo kidogo
lilimfanya awe na uzito katika kuchukua makocha wenye majina
makubwa.
Alimuacha Di Matteo na kumpa mkataba wa miaka miwili kama zawadi.
Lakini siku zote alikuwa anatafuta sababu ya kumtimua.
Wakati huo huo Torres
aliendelea kuwa na kiwango kibovu.
Torres ni mchezaji ambaye siku zote maisha
yake yamekuwa ya umimi, yakimzunguka mwenyewe tu.
Mfano mzuri tuliiona tabia
yake muda mfupi baada ya fainali ya Champions league jijini Munich.
Badala ya
kushangilia ushindi mkubwa zaidi katika historia ya Chelsea, Torres alikuwa
akilalamika kuhusu kutopewa nafasi ya kupiga penati na kuachwa kwenye benchi
akicheza kwa dakika sita tu za dakika za kawaida
Alisema: “Nimekuwa kwenye
kipindi kigumu cha maisha yangu ya soka msimu huu na sipo tayari kukirudia tena.
Msimu ujao nataka mtu aniambie nini kitatokea, jukumu lipi nitakuwa nalo kwenye
timu, nini nitegemee na nione kama kitakuwa na thamani hiyo."
Japokuwa
aliambiwa kabisa nini kitatokea na jukumu gani atakalokuwa nalo kwenye timu. Na
kumpa sapoti yote aliyotaka Abramovich akaenda kumuongezea watengenezaji magoli
wengine pembeni ya Juan Mata - Eden Hazard na Oscar.
Kama vile haikutosha
Abramovich akamruhusu Didier Drogba kuondoka ili kumpa nafasi zaidi Torres
kwenye timu.Torres akashinda vita ambayo hakufanya chochote kushinda.
Sasa,
ingawa amekuwa na nafasi ya kuonyesha nini anaweza kufanya na kulipa fadhila ya
imani anayopewa na mmiliki wa klabu lakini bado ameendelea kuwa Sheva namba
2.
Na bado Abramovich akaendelea kumsisitiza na kumuelekeza Di Matteo kwamba
Torres aanze kwenye kikosi cha kwanza. Kocha akaendelea kufuata maelekezo ya
bosi kinyume na mapenzi yake.
on Monday, November 26, 2012
Post a Comment