Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BAADA YA DIAMOND, NISHA... JB, OMMY DIMPOZ NAO WANUSA KIFO


Gari la Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ baada ya ajali.

Matukio ya wawili hayo yalitokea siku moja ya Novemba 12, mwaka huu wilayani Kinondoni, Dar. JB ilikuwa maeneo ya Namanga ambapo gari lake aina ya Toyota Verossa liligongana na pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda. Ommy Dimpoz yeye na gari lake aina ya Toyota Rav 4, Kijitonyama kwa kuvaana na basi.
Akizungumzia tukio hilo juzi wakati akiongea na paparazi wetu, JB alisema:
“Ukiniuliza jinsi ajali ilivyotokea n’tashindwa kuielezea ila ninachojua nilitoka Leaders Club kuelekea Namanga kuweka mafuta, sasa nikiwa nakata kona kuingia sheli (akimaanisha kituo cha mafuta) ghafla nikashtukia Bodaboda imevaa ubavuni mwa gari langu.


Msanii Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

“Kilichonichanganya zaidi huyo mwendesha Bodaboda akasema kumbe ni wewe JB, mimi ni shabiki mkubwa wa filamu zako dah! Maneno hayo yalinitia huzuni maana alikuwa akisema hivyo huku anavuja damu kinywani.

“Ilibidi nimkimbize Hospitali ya Muhimbili ambapo alitibiwa na kuruhusiwa. Ila namshukuru Mungu mimi sikupata majeraha zaidi ya gari langu kubonyea
kwenye mlango wa nyuma kulia.”
Ommy Dimpoz yeye alitiririka hivi: “Dah! Mwisho wa mwaka huu, kuna majanga makubwa sana, huwezi amini ajali hii ilinipata nikiwa sina hili wala lile wakati nipo kwenye moja ya mizunguko yangu.

Gari la Jacob Steven ‘JB’ baada ya ajali.
“Ila namshukuru Mungu sikuumia popote na gari langu lipo gereji linakarabatiwa, natarajia kulipata jioni ya leo (Jumanne).”
Ajali za Diamond na Nisha zilitokea Barabara ya Kimweri, Msasani, Dar usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita. Cha ajabu ni ajali hizo kuchagua mastaa wa fani tofauti, wakati Diamond ni wa Bongo Fleva, Nisha ni wa filamu kama ilivyokuwa kwa JB na Ommy Dimpoz.

Mwenyekiti wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top