Basi linalofanya safari
zake za biashara kati la Liwale na Dar es salaam leo majira ya saa sita mchana
limeua watu watano hapohapo na kuacha majeruhi wengi na watatu kati yao
kulazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi hadi sasa.
Basi hilo linalojulikana kwa jina la MCHAKATO lililokuwa linatokea Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi na kuelekea Dar es salaam limepata ajali mbaya majira ya saa 6 maeneo ya Nangulukulu na kuuwa watu watano, kuacha majeruhi kadhaa na watatu hadi sasa wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Kinyonga - Kilwa mjini.
Chanzo cha ajali bado ni kitendawili hadi sasa, Maiti za wahanga wa ajali hiyo zipo kwenye Hospitali ya Kilwa kivinje zikisubiri ndugu wa Marehemu na utaratibu wa mazishi, maiti tatu kati ya yao zimeshatambulika , moja ni ya Nesi mmoja wa Mbulu (Mrs Nyagali) aliyekuwa akitoka Liwale kwa mume wake, nyingine ni ya Mjasiriamali mmoja mwenyeji wa Bukoba aliyefahamika kama Dora Kaisiki na yatatu ni ya Mwalimu wa shule ya Msingi ya Muungano ya Liwale mjini aliyefahamika kwa jina la Frola Frances pia ni mwenyeji wa Bukoba.
Post a Comment