|
UNAHISI mwenzi wako anakusaliti
kwa maana kwamba anafanya ngono na wanawake au wanaume wengine? Fahamu kuwa wapo
wengi wenye kulalamikia hilo. Kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini hasa anatoka na wengine ikiwa
aliahidi kwamba atakuwa ananipenda milele? Wengine wanakwenda mbali zaidi na
kufikiri kila kitu ambacho anakifanya kwa mwenzi wake kitakuwa ni chenye
kumpendeza mwingine. “Mimi najitahidi
kumfanyia mambo mengi mazuri, bado anaonekana haridhiki,” ndivyo baadhi ya watu
wanavyojisemea. UKWELI UKOJE?: Ni vizuri katika mapenzi kupata muda wa
kuzungumza mwenzangu unapendelea nini na usingependa ufanyiwe
nini.KUAMINI KUWA UNAYOFANYA NI
MAZURI, BILA KUAMBIWA NA UNAYEMFANYIA, SIO SAHIHI. Maisha ya raha katika
uhusiano ni kuhakikisha kunakuwa na fursa ya wapendanao kukaa na kujadili namna
gani wamekuwa wakiishi na nini cha kufanya ili waweze kuwa na maisha bora
zaidi. KUKWAZANA NI MAMBO YA KAWAIDA
KATIKA MAPENZI. IKIWA UMEKAA KWENYE TUMBO LA MAMA YAKO NA BADO KUNA WAKATI
MNAKWAZANA, IWE MTU AMBAYE MMEKUTANA TU MITAANI?
Jambo muhimu katika ndoa ni
kuhakikisha kunakuwa na nafasi ya wanandoa kujadili hali ya ndoa yao.
Kama ilivyo katika biashara kwamba
wafanyabiashara wakati fulani wanajadili hali ya maendeleo ya biashara ili kujua
kama kuna matatizo gani nk, ni muhimu sana wanandoa kutenga muda wa kujadili
hali ya uhusiano wao. SABABU ZA WATU
KUSALITI
Wakati fulani nimekuwa nikiongea na watu wanaosaliti ndoa...baadhi yao
ukiwauliza unaonaje sasa ukaondoa kwenye ndoa na kuoana na huyo wa nje, jibu ni
kwamba hawezi kwa sababu anasaliti si kwa sababu hampendi aliyenaye, bali wakati
mwingine ni kutofautiana. Kwa mfano
katika utafiti wangu nimegundua kwamba idadi kubwa ya wanandoa waume, hawana
uhakika wa kupata tendo la ndoa kwa wakati wanaotaka, kama ilivyo kwa baadhi ya
wanawake. Tafiti ambazo nimekuwa
nikifanya pia nimegundua kuna tofauti ya mahitaji katika ndoa, kwa mfano wakati
wanaume ni wenye kuhitaji mno tendo la ndoa, furaha ya wanawake walio wengi sio
hilo wakati fulani ni uhakika wa kupatikana kwa mahitaji ya ndani na
amani. *Kutopata mapenzi ya kweli
katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye
hakumpenda.
-Wengine hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au
mwanamke hamjali, kitendo ambacho kinasababisha baadhi yao kuona kwamba suluhu
pekee ni kwenda nje ya ndoa. *Uchafu,
kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke
-Wapo wanaume na wanawake ambao
wamekuwa wachafu wa mwili na kutojipenda, kiasi kwamba ukiwa nae unahisi
kichefuchefu. Kuna wanaume na wanawake kwa mfano wanalala bila kuoga, wengine
unakuta mwingine mlevi, mwingine hanywi, kisha anarudi nyumbani anaomba
abusiwe...mhh! raha iko wapi hapa?*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa -Ingawa
wakati mwingine huwa ni uroho wa mtu, mara nyingi hata majumbani watoto kama
hawajashiba, baadhi yao hukimbilia kudowea chakula kwa jirani. *Ubize wa kazi kupita kiasi/Kusafiri
-Kuna watu wako
bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au
labda kutojua namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara,
hiyo ni mbaya kwa wanandoa. *Tamaa ya
mali: Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni
ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia
wanaume wenye magari, wenye fedha nk. *Kujifunza mambo au mitindo mipya
-Wakati mwingine
kuna wengine wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa
waoga wa kusema ukweli kwa wenzi wao juu ya yale ambayo wanayataka, matokeo yake
wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’. *Kutopata tendo la ndoa muda mrefu, labda kwa sababu
mume ana matatizo au mke ana uja uzito mkubwa ama amejifungua n.k
-Hata hivyo
kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali
wapenzi wanaweza kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au
kumfanya mwenzi wake afurahie. |
on Monday, November 5, 2012
Post a Comment