Benkya
KCB nchini imeanza kutoa mafunzo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati ili
kuwawezesha kukuza miradi na mitaji yao ya
kiuchumi.
Wakati
wa mafunzo hayo, pamoja na mambo mengine wakufunzi wa Benki hiyo wamesema nia ni
kuongezea uwelewa wa namna ya kuanzisha miradi kuendesha biashara ndogondogo na
utunzaji wa fedha benki kwa wajasiliamali hao.
Wakati wa mafunzo hayo,
pamoja na kuelimishwa masuala mbalimbali juu ya kukuza mitajio na uansishaji wa
biashara mpya, Wakufunzi Bw. Fredrick Lyimo na Bw. Francis Mandala, wamesema
benki hiyo inaendelea na mpango wake wa kuboresha huduma kwa
wateja.
Wamesema kuwa pamoja na
kutoa elimu hiyo kwa wajasiliamali, KCB Bank ambayo ina matawi katika nchi zote
tano za Afrika ya Mashariki, pia hutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya Vifaa vya
Afya, Elimu na huduma nyingine za kijamii.
Washiriki hao
wameelimishwa jinsi ya kuweza kuomba na kupatiwa mikopo pamoja na kufundishwa
jinsi ya kuitumia mikopo wanayoipata.
Akitoa elimu juu ya
biashara na namna ya kukuza mitaji, mmoja wa wakufunzi Bw. Peace Lumelezi,
amesema kuna haja ya kila mfanyabiashara kutofautisha biashara yake naya
mwingine ili kupata faida.
Amesema kuwa hata kama
biashara ya mfanyabiashara mmoja inafanana naya mwingine katika eneo moja,
lakini ni lazima kufanyabiashara makini atofautishe biashara yake hata kwa lugha
kwani wateja wanahitaji huduma bora.
Amewashauri pia
wafanyabiashara kutokwepa kodi za Serikali na kujiwekea bima ili kuepuka ajali
na hasara za majanga ya moto ama wizi.
Amewakumbusha
wajasiliamali hao mfanya biashara zao kwa kufuata taratibu na masharti ya leseni
zao na kuepuka kukwepa kodi mambo yanayoweza kupelekea kufilisiwa ama
kushitakiwa na Mamlaka ya Kodi za mapato yaani TRA kwa upande wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na ZRB kwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wameelezea changamoto mbalimbali zinazowakuta na kusema baadhi ya waomba mikopo wamekuwa wakitoa taarifa za uongo katika mabenki ili mradi waweze kupatiwa mikopo jambo ambalo halijengi uaminifu kwa taasisi za fedha.
Pamoja na kuelezea kunufaika na mafunzo hayo, washiriki hao pia wameiomba benki ya KCB hapa nchi kuangalia uwezekano wa kuongeza matawi zaidi ya kenki hiyo pamoja na kuongeza idadi za mashine za kutolea fedha yaani ATM karibu na maeneo yenye wananchi wengi.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wameelezea changamoto mbalimbali zinazowakuta na kusema baadhi ya waomba mikopo wamekuwa wakitoa taarifa za uongo katika mabenki ili mradi waweze kupatiwa mikopo jambo ambalo halijengi uaminifu kwa taasisi za fedha.
Pamoja na kuelezea kunufaika na mafunzo hayo, washiriki hao pia wameiomba benki ya KCB hapa nchi kuangalia uwezekano wa kuongeza matawi zaidi ya kenki hiyo pamoja na kuongeza idadi za mashine za kutolea fedha yaani ATM karibu na maeneo yenye wananchi wengi.
Wamesema kwa ulimwengu wa
sasa hakuna mtu anayependa kutembea na fedha nyingi mfukoni kwa kutoka eneo moja
hadi jingine kwa kuhofia kuporwa ama kuibwa kwa fedha
zake.
Wamesema kama kutakuwa na
matawi mengi ya benki ni rahisi kwa wajasiliamali kufanya biashara zao na kuweka
fedha zao benki lakini wakazichukua hata kwa kupitia katika mashine za ATM pale
wanapozihitaji kwa matumizi ya kawaida ama ya kibiashara.
Hata hivyo wamepongeza
juhudi zinazochukuliwa na Benki hiyo katika kuwaelimisha wajasiliamali bila
kujali kama ni wateja wa benki hiyo ama vinginevyo.
Wamesema elimu hiyo
imewasaidia kwa kiasi kikubwa kujitambua na jinsi ya kukuza mitaji na kuboresha
biashara zao.


Post a Comment