Waziri wa maliasili na
Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika uzinduzi wa Mkakati wa mpya
wa Utangazaji wa Kimataifa wa Utalii wa Tanzania (International Marketing
Strategy For Tanzania)mpango uliozinduliwa jioni hii na Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB) kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kujumuisha wadau
mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya utalii ambapo Waziri Kagasheki
ameuzindua rasmi.
Waziri wa maliasili na
Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akikata utepe katika kitabu kinachoelezea
mkakati wa kutangaza utalii wa utalii wa Tanzania kimataifa kutoka kulia ni Bw.
Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Ahmad
Khatib Kamishna wa Utalii na kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania
TTB Dkt. Aloyce Nzuki.
Meneja Masoko wa Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) Bw Geofrey Meena kushoto na Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Utalii Tanzania TCT Bw. Richard Rugimbana wakifuatilia kwa karibu maelezo
yaliyokuwa yakitolewa katika uzinduzi huo.
Waziri wa Maliasili na
Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa
bodi ya utalii Balozi Charles Sanga katikati na Mjumbe wa Bodi hiyo Bi. Teddy
Mapunda.
Balozi Khamis Kagasheki
akisalimiana na Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Bodi ya (TTB) Mh. Abdulkarim
Shah
Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Utalii Tanzania TCT Bw. Richard Rugimbana kulia akijadiliana jambo na Dan
Kisirye kutoka International Finance Corporation, katikati ni Godfrey Simbeye
Mkurugenzi Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania Private Sector
Foundation.
Kutoka kulia ni wafanyakazi
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTBKaraze, Beatrice na Fatma wakiwa katika picha ya
pamoja.
kundi la Wanne Star
likitumbuiza katika uzinduzi huo
Baadhi ya maofisa wa bodi
ya utalii Tanzania wakiwa katika hafla hiyo wakibadilishana mawazo hapa na pale
kulia ni Bw. Mussa Kopwe Mkuu wa Utawala, Bw. Deo Mkuu wa Utafiti kushoto na Bw.
Kaduma Mwanasheria wa (TTB) katikati.
Post a Comment