Wanajumuiya ya Kimataifa ya kujitolea TAKATOF iliyo chini ya Taasisi ya Emirate wakishirikiki ujenzi wa Majengo ya Skuli ya Mfurumatongowa iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.P(icha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Mkuu wa Msafara wa Jumuiya ya Kimataifa ya kujitolea TAKATOF iliyo chini ya Taasisi ya Emirate akielezea malengo ya jumuiya hiyo katika ziara yao ya kushiriki ujenzi wa Majengo ya Skuli ya Mfurumatongowa iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Jumla ya shilingi Milioni 25 zimetolewa na Jumuiya ya Kujitolea ya kimataifa TAKATOF iliyo chini ya Taasisi ya Emirates kwa ajili ya kuendeleza ukarabati wa Majengo ya Skuli ya Msingi ya Mfurumatonga iliyopo Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkuu wa Msafara wa Jumuiya ya TAKATOF Lujan Mourad amebainisha hayo leo wakati Wanajumuiya hiyo walipokuwa wakishiriki ujenzi wa mabanda ya Skuli hiyo ikiwa ni mfulizo wa siku sita za kujitolea Zanzibar.
Amesema Jumuiya ya TAKATOF mbali na kukarabati mabanda ya Skuli hiyo, wamekusudia kutengeneza Madawati, kukarabati Mahodhi kwa ajili ya kuhifadhia maji safi sambamba na kutengeneza Madeski kwa Madarasa matano katika Skuli ya Mfurumatongo na Kidimni.
Akizungumzia lengo la ziara yao Lujan amesema wamekuja Zanzibar kujitolea kufanya kazi za kijamii kutokana na Jamii ya Zanzibar kuwa na mahitaji muhimu ambayo Jumuiya yao inaweza kuyafanya.
Aidha ameongeza kuwa hii ni mara ya pili kuja Zanzibar kufanya shughuli za kujitolea ambapo kwa mara hii wakishirikiana na Jumuiya ya FAWE Zanzibar wamedhamiria kununua vifaa vya kujifunzia ikiwemo Madaftari,Sare na Mabegi kwa ajili ya Watoto Yatima 100 .
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Skuli ya Mfurumatongo Muumini Fumu Othman ameishukuru Jumuiya ya TAKATOF kwa kuamua kuisadia Skuli yao, jambo ambalo linafaa kuigwa kwa Jumuiya nyingine.
Ameongeza kuwa lengo la Skuli yao ni kuona kuwa Wanafunzi wote katika Skuli hiyo wanakaa katika Madawati sambamba na kuja kipindi kimoja tu cha Asubuhi badala ya kuja vipindi viwili vya Asubuhi na Jioni.
Muumin amewaomba wadau kuendelea kuisadia Skuli yao ili waweze kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na uwepo wa Madawati na Madarasa ya kutosha ili Wanafunzi waweze kujisomea katika mazingira ya kuridhisha.
Jumuiya ya Kimataifa ya TAKATOF iliyo chini ya Taasisi ya Emirate kutoka Falme za Kiarabu ipo Zanzibar kwa siku sita ambapo Jumla ya Wanachama wake 18 wakishirikiana na Wakaazi wa Mfurumatongo Unguja wanajitolea kwa ajili ya kukarabati Ujenzi wa Majengo katika Skuli ya Mfurumatongo