Mamlaka nchini Burma inakusudia kuwawapa msamaha wafungwa 452 siku chache kabla ya rais Barrack Obama wa Marekani kuitembelea nchi hiyo.
Msamaha huo utakaohusisha wafungwa wa kisiasa, unatarajiwa kusaidia kuboresha uhusiano mwema baina ya nchi hizo.
Hatua hiyo ni mpya zaidi katika mfululizo wa kuachiwa kwa wafungwa chini ya serikali ya mabadiliko ya rais Thein Sein wan chi hiyo.
Ziara hiyo ya rais Obama itakayokuwa ya kwanza kwa rais wa Marekani aliyeko madarani kutembelea Burma inatarajiwa kuongeza moyo nchi hiyo kuendelea na mabadiliko.
Hata hivyo haijawekwa wazi kuwa ni wafungwa wangapi wa kisiasa watakaoachiwa huru, huku makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu yakisema yanaamini kuwa kuna wafungwa takriban 300 wa kisiasa.
Msamaa kama huo uliotolewa mwezi Septemba ulishuhudia wafungwa zaidi ya 500 wakiachiwa huru, huku kambi ya upinzani ikisema takriban wafungwa 58 wa kisiasa waliachiwa huru