CAF imetangaza
orodha fupi ya majina ya wachezaji ambao wamo katika nafasi nzuri zaidi ya
kutwaa tuzo ya mchezaji bora zaidi barani Afrika. Mshindi wa mwaka jana, Yaya
Toure, anaongoza katika orodha hiyo yenye majina ya wachezaji 10, waliochaguliwa
kutoka orodha ndefu ya wachezaji 34.
Mchezaji huyo kutoka
Ivory Coast, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Manchester City, ni kati ya
wachezaji wanne wanaozichezea timu za Uingereza ambao huenda wakapata tuzo hiyo
ya mwaka 2012. Kiungo cha kati wa Chelsea, John Obi Mikel, mshambulizi wa
Arsenal, Gervinho, Demba Ba wa timu ya Newcastle, ni kati ya wachezaji wengine
wa ligi kuu ya Premier ambao wanawania tuzo hiyo.
Katika orodha hiyo, kuna
wachezaji wengine ambao waliwahi kucheza Uingereza mwaka 2012. Wachezaji hao ni
aliyekuwa kiungo cha kati wa Arsenal, Alexandre Song, na ambaye sasa huichezea
Barcelona ya Uhispania, na mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba,
ambaye anaichezea klabu ya China, Shanghai Shenhua.
Chris Katongo ni
mchezaji wa pekee kutoka timu ya Zambia iliyoibuka mshindi katika mashindano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika. Mchezaji wa Morocco, Younes Belhanda, yumo katika
orodha hiyo, kwa juhudi zake mapema mwaka huu, katika timu ya Ufaransa ya daraja
ya kwanza, Montpellier.
Wanaowania tuzo hiyo,
watapunguzwa hadi kufikia watatu, katika wiki ya mwisho ya mwezi Novemba. CAF
vilevile ilitangaza orodha fupi ya wachezaji watano, ambao wana nafasi ya kupata
tuzo la mchezaji bora barani Afrika, kwa wachezaji ambao hucheza kandanda yao
barani Afrika.
Katika ordha hiyo ni
pamoja na Mohamed Aboutrika, kiungo cha kati kutoka Misri, na aliyecheza katika
mechi ya Al Ahly ya klabu bingwa dhidi ya Esperance ya Tunisia, mchezo
uliokwishwa kwa sare ya 1-1 siku ya Jumapili.
Tuzo hizo, ambazo
zitakuwa pia ni kumpa zawadi kocha bora zaidi wa mwaka, na klabu bora zaidi
mwaka 2012, zitatolewa kwa washindi tarehe 20 mwezi Desemba, katika ukumbi wa
Banquet, katika ikulu ya rais, katika mji mkuu wa Ghana, Accra.
-BBC
-BBC
Post a Comment