IGP SAIDI MWEMA.
IGP Said Mwema (kushoto) na kulia Polisi
wakimshughulikia Mwandishi wa habari Marehemu Daudi Mwangosi ambaye baadae
alilipuliwa na bomu.
Tamko la chama
hicho limekuja baada ya IGP Mwema kufanya mabadiliko kwenye safu ya makamanda na
maofisa mbalimbali bila kumgusa wa Iringa, Michael Kamuhanda ambaye amekuwa
akiwekewa shinikizo la kuwajibishwa.
“IGP Mwema
anaendelea kupanga na kupangua safu yake bila kuzingatia ukweli kuwa Jeshi hilo
analoliongoza, liko katikati ya tuhuma za mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za
binadamu," alisema Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare.
Alidai: Uteuzi
wowote unaofanyika bila kuzingatia ukweli huo, hauwezi kuondoa doa kubwa
linaloandama jeshi hilo mbele ya macho ya Watanzania."
Lwakatare ambaye
alitoa maelezo hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema
Chadema ingetarajia mabadiliko ya kulisuka upya jeshi hilo kwa kubadili
makamanda na maofiosa wengine.
“Uteuzi huu wa
IGP Mwema umezidi kudhihirisha namna Serikali ya CCM inavyozidi kupalilia na
kukomaza mizizi ya tabia ya kulindana, si katika ufisadi wa mali za umma tu,
bali hata katika roho za watu, hasa raia wa kawaida," alisema
Lwakatare.
Alisema kuwa
Kamati Kuu ya Chadema pamoja na Barua ya Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe
kwenda kwa Rais, kumtaka Rais Kikwete ilimtaka awawajibishe viongozi wa juu wa
Wizara ya mambo ya ndani kutokana na mauaji yaliyotokea Arusha, Morogoro na
Iringa.
Alitaja baadhi ya matukio hayo kuwa ni Januari 5, mwaka huu ambapo watu watatu waliuwawa mkoani Arusha na mto mmoja aliyeuawa Agosti 27 mkoani Morogoro na Mwanindishi wa Habari mkoani Iringa Septemba, 2
Alitaja baadhi ya matukio hayo kuwa ni Januari 5, mwaka huu ambapo watu watatu waliuwawa mkoani Arusha na mto mmoja aliyeuawa Agosti 27 mkoani Morogoro na Mwanindishi wa Habari mkoani Iringa Septemba, 2
Post a Comment