WATU zaidi ya
wanne wameuwawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya mkahawa mjini
Mogadishu, Somalia.
Mwandishi wa BBC
mjini humo anasema kumetokea miripuko miwili mikubwa nje ya mkahawa huo uitwao
"The Village", katika mtaa wa Hodan, kati-kati ya mji.
Walioshuhudia
tukio hilo wanasema mabomu yaliripuliwa na watu waliojitolea
mhanga.
Mwezi wa Septemba
watu 14 walikufa kwenye shambulio katika mkahawa mwengine mjini Mogadishu wa
tajiri huyo-huyo.
Mwandishi wa BBC
anakumbusha kuwa mashambulio kama hayo hufanywa mara kwa mara, na baadhi yao ni
vitendo vya kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, ambao bado wanadhibiti
sehemu kubwa ya nchi.
Mashambulio
mengine hufanywa na magengi ya wahalifu na wanamgambo
Post a Comment