LONDON, ENGLAND
KOCHA wa zamani wa Chelsea na Manchester United, Dave Sexton amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, Chama cha Soka (FA) kimetangaza Jumapili.
Sexton alishinda FA Cup akiwa na Chelsea mwaka 1970 kabla kuiongoza klabu hiyo kubeba Kombe la Washindi Ulaya (sasa halipo), likiwa taji la kwanza kwa klabu hiyo barani Ulaya msimu uliofuata.
"Ni siku mbaya kwa soka ya England," alisema Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka wa FA, Trevor Brooking.
"Yeyote ambaye amefundishwa na Dave ataweza kukwambia kuwa alikuwa ni mtu wa aina gani…,” alisema Brooking.
Akiwa mchezaji, Sexton alizicheza klabu za Luton Town, West Ham United, Leyton Orient, Brighton, Hove Albion na Crystal Palace katika vipindi tofauti.
Alianza kazi ya ukocha akiwa na Orient kabla baadae kuzinoa Queens Park Rangers, Manchester United, England (U-21), Coventry City na Chelsea.
Post a Comment