Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee (aliyesimama) akiwasilisha hoja yake binafsi juu ya kusitishwa ugawaji wa ardhi kwa wa uwekezaji wageni hapa Tanzania.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Profesa Anna Tibaijuka ambaye aliunga mkono hoja ya Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee.
Na.Mwandishi wetu, Dodoma.
Serikali imeunga mkono hoja binafsi ya Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee juu ya kusitisha ugawaji wa Ardhi hadi tathmini ya kina itakapofanyika kujua kiasi cha ardhi kilichoko mikononi mwa wawekezaji wageni.
Katika kuwasilisha hoja yake binafssi Mbunge Mdee amedai kuwa kumekuwa na usumbufu mkubwa kwa wananchi kwa kufukuzwa katika maeneo yao ya makazi na ardhi yao kuuziwa wawekezaji wageni.
Amedai kuwa vitendo vya unyanyasaji vimeenea sana hapa nchini Tanzania na kuwafanya watanzania kuwa watumwa katika ardhi yao.
Hoja ya Mbunge Halima Mdee imeungwa mkono na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Profesa Anna Tibaijuka na kusema kuwa mgawaji halali wa ardhi ni wizara yake.
Profesa Tibaijuka amedai kuwa kumekuwa na utapeli mkubwa wa uuzaji wa ardhi kwa wawekezaji wageni hususani katika halmashauri za wilaya hapa nchini
Tibaijuka amesema kuwa hoja hiyo ya Mdee ni lazima ifanyiwe maazimio mawili kutoka serikali ambayo itawasilisha kauli ya serikali hapa baadaye.