Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAKATI KEMIKALI ALIYOMWAGIWA SHEIKH SORAGA IKICHUNGUZWA, WATU WAJITOKEZA KUMCHANGIA GHARAMA ZA MATIBABU

Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga akitolewa kutoka Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Best Import Zanzibar Issa Kassim Issa kushoto akimkabidhi Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali Abadallah dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga katika Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Vuga mjini Zanzibar..


Kampuni ya Best Imports Zanzibar inayojishughulisha na biashara ya uuzaji Kuku (Paja Nono) imetoa jumla ya Dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga.


Akitoa msaada huo leo kupitia kwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Issa Kassim Issa amesema wameamua kutoa mchango huo kutokana na kuguswa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Sheikh Soraga na kwamba kiasi hicho cha pesa kitatumika kusaidia matibabu yake.


Issa amesema wamiliki wa Kampuni hiyo David Aloy na Carlos Ajala wamestushwa na kitendo alichofanyiwa Sheikh Soraga ambaye ni mtu muhimu katika jamii kutokana na mchango wake mkubwa.


Ameongeza kuwa Shekh Soraga ni mtu mwenye heshima kubwa Zanzibar kutokana na shughuli zake za kila siku na kwamba kitendo alichofanyiwa kinapaswa kulaaniwa na kila mtu.


Kwa upande wake Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali Abadallah aliishukuru Kampuni hiyo kwa kuwa wa kwanza kutoa msaada wa kifedha na kuahidi kiasi hicho cha fedha kitapelekwa sehemu husika.


Aidha Katibu huyo amewaomba wananchi kumuombea Shekh Soraga apone haraka na wale wenye uwezo kuiga mfano wa Kampuni ya Best Import ili kufanikisha matibabu hayo.


Sheikh Soraga ambaye anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi ameumia sehemu za usoni,mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa Tindikali na mtu asiyejulikana wakati alipokuwa akifanya mazoezi viwanja vya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top