Rais anayeondoka madarakani
Hu Jintao ameahidi kuwa China itafanya mabadiliko ya kisiasa. Hu Jintao amesema
pia kuwa nchi hiyo italifanyia kazi suala la kurekebisha uchumi
wake.
Chama tawala nchini China
hivi karibuni kilimfukuza madarakani mmoja wa viongozi wake wa ngazi za juu Bo
Xilai kutokana na tuhuma za mauwaji na visa vya rushwa. Rais Hu Jintao amesema
kuwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ndani ya chama hicho ni lazima
yatolewe adhabu kali.
Mkutano wa chama hicha cha
kikomunisti unaoendelea kwa kipindi cha wiki moja hufanyika kila baada ya miaka
mitano na utamalizika kwa kukabidhi madaraka kwa Makamu wa Rais Xi
Jinping.
Chama kinalenga kufanya
Mageuzi yafatayo:
Mkutano maalum wa chama cha
kikomunsiti kufanyika kila baada ya mwongo mmoja
Viongozi wenye zaidi ya
miaka 68 watasataafishwa
Viongozi wapya wakuu
kutajwa.
Viongozi hao wameamuliwa
lakini bado hawajatajwa.
Mirengo ni muhimu kuliko
sera na mfumo wa uteuzi haueleweki
Post a Comment