Baada
ya ushindi
alioupata Rais Barack Obama wa Marekani
kwa tiketi
ya chama chake
cha Democratic dhidi
ya
mpinzani
wake Mitt Romney aliyekua
akiwania kiti hicho cha urais kupitia chama cha
Republican,kumekuwa
na
mitizamo tofauti tofauti ya kiimani juu ya ushindi huo wa Rais Obama.
Rais Obama akiwa na familia yake katika shamra shamra za kutoa shukrani kwa wapiga kura kwa kumpa miaka mingine minne kuliongoza taifa hilo la Marekani |
Moja
ya watu mashuhuri waliojitokeza
kuonesha
mitizamo yao wakikinzana na ushindi
wa rais
Obama ni Mchungaji Franklin Graham ambaye pia
ni mtoto wa Mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi ,Billy Graham wa
Marekani.
Mchungaji Franklin Graham |
Akiongea
na shirika la Utangazaji la Marekani CNN, Franklin Graham amesema kwamba, "
Taifa la Marekani kwa sasa linaelekea katika njia ya upotevu kutokana na ushindi
wa Rais Barack Obama" na hii ikiwa ni kutokana na msimamo
wa Rais Obama kukubaliana na kuhalalishwa kwa ndoa ya jinsia moja ambayo ni
kinyume na mpango wa Mungu wa ndoa
yamume
mmoja
na mke
mmoja.
"Kama tunaambiwa kuifuata
njia ambayo huyu Rais wetu anataka twende,nadhani itakua ndio kupotea kwetu na
uharibifu wa hili Taifa la Marekani @"Rev.Franklin
Graham
Kutoka kushoto: ni Mhubiri wa Kimataifa Billy Graham akiwa na mwanae mchungaji Franklin Graham |
katika uchaguzi huo
nchini Marekani kumekuwa na mitizamo tofauti ya kiimani katika majimbo tofauti
tofauti hususan katika suala la ndoa ambapo wanaopinga
ndoa ya jinsia moja na kutaka ndoa iwe baina ya Mume mmoja na Mke mmoja
walijikuta wakikabiliwa na
upinzani mkali katika majimbo manne nchini Marekani ambapo katika majimbo ya
Maryland na Washington walipiga kura wakitetea kuhalalishwa kwa ndoa ya jinsia
moja.
wapiga kura katika jimbo
la Minnesota wamezuia
mabadiliko ya katiba
kuingizwa katika katiba ya jimbo
hilo hususan suala la ndoa ya
jinsia moja
huku wapiga
kura katika jimbo jingine laNorth Star wakipinga
vikali ndoa
ya jinsia
moja.
Rais Barack Obama wakati akitoa speech yake baada ya ushindi wake |
majimbo
mengine ni pamoja na jimbo
la Maine ambapo wao wameafiki mabadiliko yanayoruhusu ndoa ya
jinsia moja
mabadiliko
ambayo yalikuwa yakipingwa kwa muda
mrefu
katika jimbo
hilo.
hiki ndicho alichokisema mchungaji Franklin Graham. "God instituted marriage. And for the president to now back something that is against God's position and – is a big problem for him with not only Evangelical churches, but African-American churches across this country who are very conservative," @ Franklin Graham.
baadhi ya matukio yaliyojiri baada ya ushindi wa Rais Obama ni kama inavyoonekana hapa chini
Post a Comment