Mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akitoa angalizo wakati wabunge walipokuwa wakitoa maoni kwenye tume hiyo ofisi za bunge mjini Dodoma leo.Kushoto ni Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda.
Wabunge leo walipata wakati mgumu wakati walipokuwa wakitoa maoni yao kuchangia maoni ya katiba mpya mbele ya tume ya kukusanya maoni ya katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Wabunge wengi waliochangia maoni yao walikutwa wakibamizwa maswali makali kutoka kwa mwenyekiti huyo wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya.
Baadhi ya wabunge walishindwa kufafanua hoja zao huku wachache wakifanikiwa kujenga vizuri hoja yao ya kuboresha masuala mbalimbali yaliyomo katika katiba ya sasa.
Mbunge wa Nzega , Dk Khamisi Kigwangala na Mbunge wa Nyamagana waliweza kutetea vizuri hoja ya kumpunguzia madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania hususani katika kuteua majaji na mawaziri ambapo Rais huteua Jaji Mkuu na majaji wengine wakati Rais pia huteua mawaziri kutokana na wabunge.
Wabunge hao wanadai kuwakumekuwepo na uwajibikaji mdogo kutoka kwa majaji na mawaziri wanaoteuliwa na Rais kwa vile mhimili ya Mahakama na Bunge iliwekwa kwa ajili ya kuikosoa na kuisimamia serikali iliyopo madarakani.
Wabunge hao pia walitaka mgombea binafsi apewe ruhusa ya kugombea udiwani, ubunge na urais kwa sababu watanzania wengi wapigakura walikuwa hawana vyama vya siasa, kwa hiyo katiba ya sasa inawanyima haki ya kupigiwa kura na badala yake inawapa haki ya kupigia kura watu wengine.
Post a Comment