Mtaalam
na mshauri aliye
kwenye jopo la majadiliano kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership) Prof. Lucian
Msambichaka akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam
kuhusu umuhimu wa mkutano wa kimataifa wa majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart
Partnership) kwa watanzania. Mkutano huo utafanyika nchini mwezi mei
2013.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Ushindani la Biashara Tanzania (TNBC) Bw. Samson Chemponda
akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa mkutano wa
majadiliano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership) na namna utakavyowawezesha
watanzania kubadilishana uzoefu kutoka kwa wataalam kutoka nchi nyingine kuhusu
matumizi ya teknolojia kuondoa umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo kwenye
maeneo yao.
Baadhi
ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye semina kuhusu majadiliano
kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership) na nafasi ya vyombo vya habari
katika kukuza
na kuimarisha uchumi na kuongeza uelewa miongoni mwa wananchi kuhusu nafasi na
fursa walizonazo katika kukuza uchumi nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mkutano wa kimataifa wa majadiliano ya pamoja utakaofanyika nchini mwezi Mei
2013.
Meneja Mradi wa Majadiliano kwa
manufaa ya wote (Smart Partnership) Bi. Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari kuhusu namna ambavyo wadau takribani 800 kutoka
mataifa mbalimbali watakutana nchini Tanzania kujadili kwa pamoja changamoto za
kimaendeleo, kiteknolojia na namna wananchi watanufaika kutokana na kutengeneza
mtandao wa kutafuta suluhisho la matatizo ya kiuchumi kutoka pande
zilizofanikiwa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
Post a Comment