Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali, George Waitara
(kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo juu ya maandalizi ya upandaji mlima Kilimanjaro unaotaraji kufanyika Desemba
6, 2012. Jenerali Waitara ndiye atakae ongoza upandaji huo wa mlima
Kilimanjaro.Miongoni mwa taasisi na makampuni ya liyodhamini upandaji huo wa
mlima Kilimanjaro ni Kampuni ya Bia ya Serengeti, Precision Air, JWTZ, Jeshi la
Magereza , KJ Traders and General Supplies Ltd na Kibosho resort.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali, George Waitara
(kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo juu ya maandalizi ya upandaji mlima Kilimanjaro unaotaraji kufanyika Desemba
6, 2012. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB, Balozi Charles
Sanga na Mratibu wa Upandaji wa Mlima Kilimanjaro, Joseph Kitani. Jenerali
Waitara ndiye atakae ongoza upandaji huo wa mlima
Kilimanjaro.
*******
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUPANDA MLIMA KILIMANJARO TAREHE 06 DESEMBA 2012,
IJULIKANAYO KAMA “ANNUAL KILIMANJARO
CLIMB”
Kampuni ya KJ
Traders ikishirikiana na Tanzania Tourist Board (TTB) imeandaa Uhuru expedition
ambayo ni mwendelezo wa kumbukumbu ya kutangaza Mlima Kilimanjaro kwa
kuwashirikisha watu mbalimbali wakiongozwa na Jenerali Mstaafu George
Waitara.
Utaratibu wa
expedition hiyo ulianza mwaka 2008 wakati huo ukiratibiwa na M/S KJ Traders na
Kibosho Resort, lakini kwa sasa baadhi ya taasisi za Serikali na Mashirika ya
Umma nao wameingia na kuleta msisimko mpya kwa nia kukuza utalii kwa kutumia
Mlima Kilimanjaro.
Expedition hiyo
ya kupanda Mlima inatarajiwa kuanza tarehe 06 Desemba 2012 na kuhitimishwa
tarehe 10 Desemba 12, na Waziri wa Maliasili na Utalii atahitimisha rasmi tukio
hilo.
Makampuni na
Taasisi za Umma ambazo zinatarajia kwa udhamini na ushirika katika tukio hilo ni
o
Tanzania Tourist Board
(TTB)
o
Jeshi la Wanachi wa
Tanzania
o
Serengeti Breweries
Ltd
o
Jeshi la
Magereza
o
NMB
o
KJ Traders and General
Supplies Ltd
o
Kibosho
Resourt
Watu wanaotarjiwa
kupanda Mlima safari hii ni Wabunge, baadhi ya wanajeshi na wananchi wa kawaida.
Vilevile tunarajiwa kupata Mgeni kutoka nje ya nchi mwanachi wa Tibeti
(China).
Kauli mbiu yetu
mwaka huu ni “KUKUZA UTALII NA KUTUNZA MAZINGIRA KWA ULINZI
SHIRIKISHI”.
Wote
mnakaribishwa.
Jenerali Mstaafu
George Waitara
Post a Comment